Timu ya Simba imesema Mganda Hamisi
Kiiza atakuwa chachu ya mafanikio katika msimu ujao baada ya kusaini
mkataba wa miaka miwili Kiiza amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea
Simba ya Tanzania katika msimu ujao wa ligi kuu Tanzania Bara.
Kiiza
aliichezea timu ya Yanga, ambayo ni mahasimu wa Simba katika msimu
uliopita na baadae klabu hiyo kuamua kuachana naye. Habari kutoka SImba
zinasema wana imani mchezaji huyo ataisaidia timu hiyo iliyomaliza
nafasi ya tatu katika msimu uliopita na ikiwa na kiu ya kushiriki
michuano ya kimataifa, baada ya kutoshiriki kwa miaka kadhaa. Awali,
Kiiza alihusishwa na timu ya Mbeya City lakini msemaji wa Simba, Haji
Manara amenukuliwa akisema wamemalizana na Mganda huyo, aliyejiunga kama
mchezaji huru
Home
»
»Unlabelled
» ISOME HII YA KIIZA KUTUA RASMI SIMBA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment