SAM_3481
Aliyesimama ni Mwenyekiti wa Taifa wa umoja wa wasambazaji wa kazi za Sanaa nchini, yaani ‘Tanzania Audio Visual Works Distributors,’ Baraka Nyanda akiongea na waandishi wa habari jijini Arusha juu ya kushuka kwa ubunifu miongoni mwa wasanii nchini ambako kumepelekea uwepo wa sinema na miziki hafifu isiyoweza kusahimili ushindani wa soko la kazi za burudani duniani anayefatia ni katibu wa shirika hilo Frank Martin ,watatu ni James Mollel katibu tawi laArusha pamoja na Gabriel Simbeye mjumbe.
SAM_3485
katibu wa shirika la Tanzania Audio Visual Works Distributors Frank Martin amebainisha kuwa tasnia ya filamu na muziki nchini ilikuwa na mafanikio kuanzia mwaka 2005 ambapo kazi Zaidi ya 300 zilikuwa zinafyatuliwa kila mwaka kwa mujibu wa ripoti ya Media for Development International ya 2011.
SAM_3493
Mwandishi wa habari kutoka Daily News Marc Nkwame akiuliza swali.(VICTOR)
SAM_3497
Simon Mwapangala maarufu kama ‘Rado,’akizungumzia hali halisi ya kushuka kwa soko la sanaa hapa Nnchini ambapo alisema kuwa hata kampuni za usambazaji filamu zinachangia kuua tasnia hiyo kwa kuwapa waandaaji malipo finyu.
Muziki na Filamu zinazorekodiwa nchini zinadaiwa kupoteza umaarufu nchini kiasi cha kusababisha soko lake kuangukia pua, huku waandaaji na wasambazaji wake wengi wakiamua kujitoa na kutafuta shughuli zingine za kufanya.
Mwenyekiti wa Taifa wa umoja wa wasambazaji wa kazi za Sanaa nchini, yaani ‘Tanzania Audio Visual Works Distributors,’ Baraka Nyanda, pamoja na katibu wa shirika hilo Frank Martin wamelaumu kushuka kwa ubunifu miongoni mwa wasanii nchini ambako kumepelekea uwepo wa sinema na miziki hafifu isiyoweza kusahimili ushindani wa soko la kazi za burudani duniani.
“Tathmini kutoka wasambazaji waliochini ya ‘Tanzania Audio Visual Works Distributors,’ ambao wanafikia 200 kwa sasa, imeonesha kupungua kwa kazi za Sanaa yaani muziki na filamu kwa asilimia Zaidi ya 50 na hii imesababishwa na kukosekana kwa masoko ya kazi hizo nchini,” alisema Katibu wa chama hicho, Frank Martini.
LIKE PAGE YETU HAPO PIA SHARE STORY NA RAFIKI ZAKO

0 comments:

 
Top